UN imesitisha usafirishaji misaada baada ya magari yake kushambuliwa Aleppo

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Malori ya Umoja wa matifa yalioshambuliwa Aleppo

Umoja wamataifa umesitisha misafara yote ya misaada nchini Syria baada ya malori ya Umoja huo kushambuliwa na ndege za kivita karibu na Aleppo Jumatatu.

Msafara huo ulipkea vibali vinavyostahili na pande zote katika mzozo zikiwemo Urusi na Marekani ziliarifiwa, amesema msemaji wa Umoja wa mataifa.

Malori 18 kati ya 31, yaliobeba ngano, nguo za baridi na dawa, yaliharibiwa.

Wanaharakati kutoka shirika la uangalizi Syria lililo na makao yake Uingereza linasema magari hayo yameshambuliwa na ndege za kivita za Syria au Urusi.

Afisa mkuu wa shirika la misaada la Syrian Arab Red Crescent ni miongoni mwa raia kadhaa waliouawa.

Haki miliki ya picha SYRIA CIVIL DEFENCE WHITE HELMETS/AP
Image caption Mwanaharakati anaonyesha eneo linalosemekana kushambuliwa

Marekani imeghadhabishwa na shambulio hilo, lililotokea katika mji wa Urum al-Kubra saa chache baada ya jeshi la Syria kutangaza makubaliano ya kusitisha mapigano yalioidhinishwa na Marekani na Urusi.

Marekani imesema ''itakakgua upya uwezekano wa siku zijazo wa ushirikiano " na Urusi - mshirika wa serikali ya Syria.

Usafirishaji wa misaada katika maeneo yaliozingirwa yalikuwa ni sehemu muhimu ya makubaliano ya kusitisha uhasama yaliofikiwa wiki iliopita.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii