Muhubiri anayepinga mapenzi ya jinsia moja afurushwa Botswana

Muhubiri wa Marekani Steven Anderson kufurushwa nchini Botswana
Image caption Muhubiri wa Marekani Steven Anderson kufurushwa nchini Botswana

Muhubiri mwenye utata anayepinga mapenzi ya jinsia moja kutoka Marekani Steven Anderson anafurushwa nchini Botswana na kurudishwa kwao Marekani.

Kulingana na gazeti la Mmegi katika ukurasa wake wa facebook,muhubiri huyo kwa sasa anazuiliwa katika idara ya uhamiaji na anangojea kurudishwa makwao.

Wiki moja iliopita Afrika Kusini ilimzuia bwana Anderson kutozuru taifa hilo kutokana na matamshi yake ya ukosoaji kuhusu mapenzi ya jinsia moja.

Waziri wa maswala ya ndani nchini humo anasema kuwa alikatazwa viza kwa sababu katiba ya taifa hilo inapinga matamshi ya chuki.

''Ninawaonea huruma watu wanaoishi Afrika Kusini,lakini nashkuru Mungu ,tuna fursa kubwa nchini Botswana'' ,Anderson alichapisha katika ukurasa wake wa facebook baada ya uamuzi wa kumkataza viza.