Waathiriwa wa Samsung Galaxy Note 7 wabadilishiwa simu

Samsung Galaxy Note 7
Image caption Samsung Galaxy Note 7

Simu ya Samsung Galaxy Note 7 iliodaiwa kuwa na betri zinazolipuka imeanza kubadilishwa Uingereza.

Kampuni ya Samsung inataka wamiliki wa simu hizo walioathirika kuwajulisha waliowauzia,lakini wengi wa wafanyibiashara wa simu hizo wanasema tayari wanawasialiana na wateja wao moja kwa moja.

Simu hizo zilitakikana kurudishwa kufuatia ripoti duniani kwamba betri zake hulipuka zinapopata chaji .

Samsung inatoa simu za bure kwa wale walioathirika huku wafanyibiashara wa simu hizo wakipata mali mpya huku simu zaidi zikiendelea kufikishwa sokoni katika kipindi cha wiki mbili zijazo.

Image caption Simu aina ya Samsung Galaxy Note 7 iliolipuka

''Tumetoa wito kwa waathiriwa wa simu hizo kuzibadilisha haraka iwezekanavyo.Simu ya galaxy Note 7 zenye betri ishara ya betri ya kijani zilikuwa salama kutumia'',Samsung imesema.