Obama: Magari yanayojiendesha kuokoa maisha

Marekani yatoa maelezo ya kusimamia magari yanayojiendesha Haki miliki ya picha Thinkstock
Image caption Marekani yatoa maelezo ya kusimamia magari yanayojiendesha

Serikali ya Marekani imechapisha maelezo ya kusimamia ongezeko la magari yanayojiendesha nchini humo.

Orodha hiyo ya maelezo 15 inazungumzia usalama wa magari hayo,mfumo wa magari , pamoja na kurekodi na kusambaza data.

Katika chapisho la gazeti moja ,rais Obama amesema kuwa magari yanayojiendesha yamepiga hatua ya kuwa hali halisi inayojitokeza baada ya kuonekana kuwa ndoto hapo awali.

Amesema kuwa magari hayo yanaweza kuokoa maisha ya wengi pamoja na wale wasioendesha magari kwa sasa.

Muungano wa watengenezaji magari umeunga mkono hatua hiyo ukisema kuwa magari hayo yanaweza kusaidia kuzuia mgogoro wa sheria tofauti zilizopo katika majimbo mbalimbali.