George HW Bush kumpigia kura Clinton

Bush na mkewe Barabara hawajamuidhinisha Donald Trump kuwania urais Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Bush na mkewe Barabara hawajamuidhinisha Donald Trump kuwania urais

Aliyekuwa rais wa zamani wa Marekani kupitia tiketi ya chama cha Republican George HW Bush amesema kuwa atampigia kura mgombea wa urais kupitia tiketi ya Democrat Hillary Clinton .

Bwana Bush amedaiwa kutoa ahadi hiyo kwa Kathleen Kennedy Townsend, mpwa wa rais wa zamani nchini humo John F Kennedy.

Afisi ya rais huyo wa zamani imethibitisha ripoti hiyo huku msemaji wake akisema anaingalia.

Bwana Bush aliyetawala kutoka mwaka 1989 hadi 1993 hajamuidhinisha mgombea wa urais kupitia chama cha Republican Donald Trump .

Vilevile mwanawe,Jeb Bush,ambaye alishindwa katika kinyanganyiro cha urais kupitia tiketi ya chama hicho mbali na wapinzani wengine katika kinyanganyiro hicho ,Ted Cruz na John Kasich.

Bi Kennedy Townsend ,aliyekuwa luteni Gavana wa Maryland alichapisha picha katika Facebook akiwa katika mkutano na George HW Bush ikiwa na maelezo :''Rais ameniambia atampigia kura Hillary''!