EU kujadili vikwazo dhidi ya DRC

Waziri wa maswala ya kigeni nchini Ufaransa Jean-Marc Ayrault
Image caption Waziri wa maswala ya kigeni nchini Ufaransa Jean-Marc Ayrault

Muungano wa Ulaya EU unatarajiwa kujadiliana kuhusu uwezekano wa kuiwekea vikwazo Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo,waziri wa maswala ya kigeni wa Ufaransa Jean-Marc Ayrault amesema kulingana na chombo cha habari cha Reuters.

Alipoulizwa iwapo angetaka vikwazo kama vile vya Marekani kuwekwa kwa kile ilichotaja ukandamizaji wa upinzani ,Reuters ilimnukuu Bwana Ayrault akisema:

''Ni swala tutakalozungumzia lakini hali inatia wasiwasi na ni hatari sana''.

Marekani tayari imetishia kuwawekea vikwazo baadhi ya wanasiasa kwa kuchelewesha kufanyika kwa uchaguzi,unaotarajiwa mwezi Novemba.