Angelina Jolie na Brad Pitt kutalikiana

Angelina Jolie na Brad Pitt Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Angelina Jolie na Brad Pitt wamekuwa pamoja tangu 2004

Wanandoa maarufu zaidi wa Hollywood, Angelina Jolie na Brad Pitt, wanatarajiwa kutalikiana karibuni.

Wakili wa Angelina Jolie, Robert Offer, amesema Jolie ndiye aliyeanzisha shughuli hiyo.

Tovuti ya habari za wasanii mashuhuri ya T-M-Zee imesema Jolie aliwasilisha nyaraka za kuomba talaka kortini Jumatatu, akitaja tofauti ambazo haziwezi kusuluhishwa.

Tovuti hiyo inasema ameomba kusalia na watoto wao sita.

Wawili hao walifunga ndoa Agosti 2014, maiaka kumi baada yao kuanza kuchumbiana.

Watoto wao sita ni Maddox, Pax, Zahara, Shiloh, napacha Knox na Vivienne.