Bosco Ntaganda aanza kula baada ya kugoma wiki mbili ICC

Bosco Ntaganda Haki miliki ya picha AFP
Image caption Kiongozi wa zamani wa waasi DRC anakabiliwa na mashtaka 18

Aliyekuwa kiongozi wa waasi katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Bosco Ntaganda ameanza kula baada ya kugoma kwa takriban wiki mbili katika kizuizi chake kwenye mahakama ya kimataifa ya uhaini huko Hague, Shirika la AFP linaripoti..

Anakakabiliwa na kesi ya uhalifu wa kivita.

Amepewa jina la utani "The Terminator" kutokana na shughuli zake Congo, Ntaganda aligoma kula kulalamika dhidi ya hali inayomkabili kizuizini, ikiwemo kuhusu suala la kutembelewa na familia yake.

AFP imemnukuu wakili wake Stephane Bourgon aliyesema kwamba ameanza tena kula.

Ameongeza:

''Iwapo kila kitu kitakwenda sawa, mkewe atafika The Hague kuanzia Alhamisi na ataweza kumuona bwana Ntaganda kwa kiwango fulani cha faragha, kitakachokidhi matarajio yake."

Mwaka jana, Ntaganda alikana mashtaka 18 yanayomkabili - ikiwemo mauaji, kuwasijili watoto katika jeshi na kuwatumia wanawake kama watumwa wa ngono.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii