Miaka 3 baada ya shambulio la Westgate
Huwezi kusikiliza tena

Maswali mengi yamesalia miaka 3 baada ya shambulio la Westgate

Miaka mitatu kama leo, wanaume waliojihami kwa bunduki walivamia jumba la biashara la Westgate, katikamtaa wa kitajiri mjini Nairobi.

Ni mojawapo wa mashambulio mabaya kuwahi kushuhudiwa lililotekelezwa na wanamgambo wenye itikadi kali Afrika mashariki.

Watu 67 waliuawa na wengine 175 walijeruhiwa.

Hii leo bado kuna maswali mengi yaliosalia, kama ni washambuliaji wangapi waliohusika, na kwanini shambulio hilo liliweza kuendelea kwa siku tatu.

Rais Uhuru Kenyatta ameahidi kuunda tume ya uchunguzi kusaidia kutafuta jibu kwa maswali hayo lakini bado haijakutana.