Wahudumu 4 wa afya wauawa kwa makombora Aleppo

Kumeshuhudiwa mashambulio ya makombora mashariki mwa Aleppo pia Haki miliki ya picha AFP
Image caption Kumeshuhudiwa mashambulio ya makombora mashariki mwa Aleppo pia

Wahudumu 4 wa afya na waasi 9 wameuawa karibu na Aleppo wakati makombora ya angani yalipofyetuliwa usiku na ndege za kivita za Syria na Urusi shirika la uangalizi la haki za binaadamu Syria limesema Jumatano.

Inafahamika kwamba makombora yameulenga mji wa Khan Touman, unaodhibitwana waasi kusini magharibi mwa Aleppo.

Wahudumu hao wa afya wanayafanyia kazi mashirika ya usaidizi ya Union of Medical Care na Relief Organizations, yaliothibitisha vifo hivyo.

Inadhaniwa kuwa maafisa hao wa afya waliitwa katika zahanati moja kuwachukuwa wagonjwa kadhaa kwa matibabu maalum.

Zahanati hiyo imeharibiwa kabisaa, na inahofiwa kuwa kuna watu zaidi waliouawa au kuzikwa chini ya vifusi.

Waasi hao 9 wa kutoka Jaish al Fatah - kundi la wanamgambo wa kiislamu ambayo siyo sehemu rasmi ya muungano unaoungwa mkono na mataifa ya magharibi, lakini ni kitengo kinachohudhumu sambamba na jeshi linalopigania uhuru wa Syria.

Haijulikani ni nani aliyetekeleza shambulio hilo, lakini kundi la waasi limelengwa na ndege za kivita za Syria na Urusi katika siku za nyuma.