Watuhumiwa kuvuruga ushahidi katika kesi ya Tulisa

Mazher Mahmood na Alan Smith wamekana mashtaka Haki miliki ya picha JULIA QUENZLER
Image caption Mazher Mahmood na Alan Smith wamekana mashtaka

Mwandishi habari wa siri Mazher Mahmood amepanga kubadili kauli ya shahidi katika kesi dhidi ya muimbaji Tulisa Contostavlos, Mahakama ya Old Bailey imeelezewa.

Mwandishi huyo anayetambulika kama shekhe bandia na dereva wake Alan Smith wote wamekana kupanga kwa pamoja kwa lengo la kubadili mkonodo wa sheria.

Bi Contostavlos ameshutumiwa kwa kuuza bangi lakini kesi dhidi yake ilitupiliwa mbali mwaka 2014.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Muimbaji Tulisa Contostavlos

Waendesha mashtaka wanasema Mahmood alikuwana maslahi binafsi katika kushtakiwa kwake.

Wakili Sarah Forshaw amesema: "kesi ya Juni 2014 imemuanika Mahmood na taaluma yake ya uandishi katika kesi hii.

"alipenda kujiita 'king of sting', alijigamba kwenye kitabu alichoandika kuhusu idadi ya kesi alizohusika nazo binafsi.

Mahmood, mwenye umri wa miaka 53, kutoka Purley, London kusini , alitoa ushahidi uliosababisha kukamtwa bi Contostavlos na kushtakiwa kwa kuhusika katika uuzaji wa madawa ya kulevya.

Muimbaji huyo maarufu anatuhumiwa kupanga kumuuzia Mahmood bangi kupitia mojawapo ya watu wake yenye thamani ya £800.