''Bahati mbaya'' yamfuta kazi mkuu wa habari Misri

Generali Sisi alichukua uongozi baada ya mapinduzi mwaka 2013 Haki miliki ya picha AFP
Image caption Generali Sisi alichukua uongozi baada ya mapinduzi mwaka 2013

Runinga ya taifa la Misri imempiga kalamu mkuu wa idara ya habari, Mostafa Shehata, baada ya mazungumzo yake na Rais Addul Fattah Al- Sisi kuonyeshwa kwa bahati mbaya, shirika la habari la AFP limeripoti.

Kituo cha channel 1 kilipeperusha mazungumzo ya Jenerali Sisi na kukabidhi mazungumzo hayo kwa kituo cha habari cha Marekani cha PBS mwaka jana na si mwaka huu. Wameongezea kwamba matangazo hayo yalisimamishwa pindi tu wafanyikazi walipogundua yalipeperushwa hewani kwa bahati mbaya.

Bwana Shehata, aliambia kituo cha habari cha AFP kwamba kufutwa kwake 'hakuna msingi wowote' kwani wengine walihusishwa katika matangazo hayo

Makosa hayo yalipingwa na watangazaji wanaounga mkono runinga ya kibinafsi ambayo imekuwa ikiangazia ziara yake alipozuru New York katika mkutano mkuu wa Umoja wa Mataifa.