Abiria 6 'walevi' wapigwa marufuku kuabiri ndege ya Jet2

Ndege ya JET 2 Haki miliki ya picha Getty Image
Image caption Ndege iliokataa kuwabeba abiria 'walevi' wasumbufu

Shirika moja la ndege limewapiga marufuku watu sita kuabiri ndege yao wakisema walikuwa walevi wenye kiburi ,wajeuri, na kubishana ovyo na wahudumu wa ndani ya ndege hiyo.

Shirika hilo liitwao Jet2 limesema vitendo vya kundi hilo la walevi sita walibughudhi safari ya ndege iliyokuwa inatoka miji ya Uingereza Newcastle hadi Tenerife hapo Jumamosi.

Zaidi ya hayo shirika hilo liliwapiga marufuku watatu wa hao kwa mwaka mmoja, lakini likakataa katakata kuwapa huduma ya usafiri wengine watatu waliokuwa wanataka kuondoka kutoka kisiwa kimoja cha watalii ili kurudi makwao.

Msemaji wa shirika hilo la ndege amesema watu hao walikuwa wamelewa chakari hata kabla ya kuabiri ndege hiyo.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Baadhi ya 'walev' hao wasumbufu walikwama baada ya kunyimwa usafiri kutoka eneo la Tenerife

Msemaji huyo amenukuliwa kusema; "Watu hao walikuwa walevi wajeuri na kutaka kuanzisha ugomvi na wahudumu wetu wa ndani ya ndege . Ni sharti waelewe kuwa matendo kama hayo ya hasa kuwabughudhi wateja wetu wengine hayawezi kamwe kukubalika na sharti wajue madhila ya kufanya ushari kama huo.

"Tungependa wateja wetu wafurahi kwa kusafiri kwa amani na utulivu bila kubughudhiwa na watu wachache wasumbufu, nasi tutafanya kila juhudi kuhakikisha tabia hiyo inakoma."