Rais Duterte aushutumu Muungano wa Ulaya

Rais Rodrigo Duterte
Maelezo ya picha,

Rais Rodrigo Duterte

Rais wa Ufilipino Rodrigo Duterte ameushutumu Muungano wa Ulaya baada ya bunge la muungano huo kukashifu kile ilichokitaja kuwa mauaji ya kiholela nchini humo.

Akitoa taarifa yake iliojaa ishara za ujeuri, bwana Duterte alisema kuwa Muungano wa Ulaya unajiondolea lawama na kwamba mataifa ya ukoloni kama vile Ufaransa na Uingereza walikuwa wakijaribu kujiepusha na madhambi yao wenyewe walioyafanya.

Ameongezea kwamba hata iwapo ripoti ya mauaji hayo ya kiholela ni ya kweli ,waathiriwa ni wahalifu.

Awali mwezi huu ,rais Obama alikatiza mkutano wake nma rais huyo baada ya ya Kumwita mwana wa kahaba.