Hali ya hatari imetangazwa katika mji wa Marekani

Familia wanasema Bwana Scott alikuwa anasoma kitabu alipouawa, lakini polisi wanasema alikuwa amebeba silaha Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Familia wanasema Bwana Scott alikuwa anasoma kitabu alipouawa, lakini polisi wanasema alikuwa amebeba silaha

Gavana wa jimbo la North Carolina ametangaza hali ya hatari katika mji wa Charlotte, wakati ghasia zinaendelea kufuatia polisi kumuua mwanamume mweusi.

Ghasia zilizuka kwa usiku wa pili baada ya kuuawa Keith Lamont Scott kwa kupigwa risasi na afisa mweusi Jumanne.

Muandamanaji mmoja yupo katika hali mahututi baada ya kuzuka ufyetulianaji risasi baina ya raia, maafisa wa mji walisema.

Bwana Scott was ni mwanamume wa tatu raia wa Marekani mwenye asili ya kiafrika kuuawa na polisi katika wiki moja.

Mauaji haya yamesbabisha maandamano makubwa katika siku za hivi karibuni

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Polisi wametumia gesi ya kutoa machozi kupambana na waandamanaji

Polisi ya kupmabana na fujo imetumia gesi ya kutoa machozi walipokabiliana na mamia ya waandamanj. Idara ya polisi inasema maafisa wake wanne wamejeruhiwa.

Awali Gavana wa North Carolina Governor Pat McCrory amesema ameanzisha jitihada kutuma jeshi la ulinzi na maafisa wa polisi wa trafiki kusaidia kukabiliana na maandamano hayo.

"ghasia zozote zinazoelekezwa dhidi ya raia wetu au maafisa wa polisi au kusababisha uharibifu wa mali hazikubaliki," alisema.

Waandamanji wana hasira kuwa bwana Scott, mwenye umri wa miaka 43, ameuawa na Polisi Jumanne mchana katika hali ya kutatanisha karibu na eneo la makaazi.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii