Kwa Picha: Miaka ya Pitt na Jolie wakiwa pamoja
Tizama maisha ya Brad Pitt na Angelina Jolie walipokuwa pamoja wakati hisia mbali mbali zinaendelea kuibuka kufuatia tangazo kuwa Jolie ametaka talaka baada ya kuwa pamoja kwa miaka 12.
-
PA
Uhusiano wa Jolie na Pit umevutia wengi katika vyombo vya habari kimataifa.
-
AP
Walifurahia kuwepo katika maonyesho ya filamu zao pamoja ikiwemo filamu ya Ocean's 13 aliyoigiza Pitt 2007.
-
Reuters
Jolie akiwa mja mzito wa pacha wao Knox na Vivienne alipohuhuduria tamasha la filamu la Cannes 2008.
-
EPA
Wapiga picha kazini: wana ndoa hawa waliwavutia wengi kokote walikokwenda.
-
Getty Images
2010 Jolie alizuru Bosnia kama balozi mwema katika UNHCR pamoja na mumewe Pitt [ameipa picha mgongo].
-
Getty_AFP
Pitt na Jolie wana watoto 6 pamoja wakiwemo 3 walio wa asili.
-
AFP/Getty
Jolie alihudhuria mkutano wa kimataifa wa kupinga unyanyasaji wa kingono katika mizozo London Juni 2014, katika wadhifa wake wa mjumbe maalum wa UN.
-
Reuters
Wameigiza pamoja katika filamu By the Sea na wanaonekana hapa wakiwasili katika kuonyeshwa mara ya kwanza filamu hiyo Hollywood Novemba 2015.
-
Reuters
Pitt na Jolie walijitambulisha rasmi kama wapenzi 2004, na wakaoana miaka 10 baadaye - mwaka picha hii ilipopigwa.
-
AP
Taarifa za kutalikiana kwao zimejiri wakati kukiwa na ripoti kuwa Jolie anataka akabidhiwe watoto wao 6 awalee huku Pitt apewe haki ya kuwatembelea. wanaonekana katika picha hii Novemba 2015.
Picha
Wekundu wa lawaridi
- 15 Februari 2019
Kwa Picha: Shambulio la Hoteli ya DusitD2 Nairobi
- 15 Januari 2019
Vitu vya ajabu vilivyogunduliwa katika makaburi Misri
- 22 Novemba 2018