Wakili afungwa jela miaka 12,China

Xia Lin Haki miliki ya picha AP
Image caption Wakili wa kutetea haki za kinadamu Xia Lin

Wakili anayetetea haki za kibinadamu amefugwa jela kifungo cha miaka 12 jambo ambalo wafuasi wake wanasema ni njia ya kumnyamazisha.

Xia Lin, ambaye mteja wake ni msanii Ai Weiwei, alipatikana na hatia ya udanganyifu ya kupata dola elfu mia saba kwa ajili ya kulipa deni lake la uchezaji kamare.

Mwaka jana China iliwakamata mamia ya mawakili, jambo ambalo wachanganuzi walisema ni ukandamizaji uliopangwa.

Mawakili wengi wameachiliwa huru lakini wengine bado wamesalia kizuizini , huku familia za mawakili hao wakinyimwa fursa ya kuwaona.

Lakini marafiki wa wakili huyo wamesema walimkabidhi wakili huyo kwa hiari.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mkewe wakili , Bi Lin Ru

Mkewe, Lin Ru amesema anaamini mumewe hana hatia yoyote kwa hivyo wanahitaji kukata rufaa.

Watetezi wa wakili huyo wa haki za kibinadamu wamesema kifungo hicho ni ulipizaji kisasi dhidi ya mtetezi wa sheria.

Hakujakuwepo na maoni yoyote kutoka kwa mahakama hiyo.