Waandamana tena Marekani kupinga mauaji

Usafi baada ya Maandamano Haki miliki ya picha AP
Image caption Usafi baada ya Maandamano

Mamia ya waandamanaji wamekusanyika kwa usiku wa tatu mfululizo, kwenye mji wa Charlotte Marekani kufuatia kuuawa kwa mtu mweusi akiwa mikononi mwa polisi.

Wengi wanataka kutolewa video inayoonyesha mwanaume huyo akipigwa risasi.

Polisi wameionyesha familia ya marehemu video, hiyo lakini wakasema kuwa hawataitoa kwa umma.

Mkuu wa polisi katika mji wa Charlotte anasema video hiyo haionyeshi kuwa Keith Lamont Scott alikuwa na bunduki mkononi wakati aliuawa.

Familia yake nayo inasema kwa ni vigumu kutambua alichokuwa nacho mkononi wakati huo.