Mahakama ya katiba Gabon kuamua matokeo ya uchaguzi mkuu

Rais Ali Bongo akipiga kura katika uchaguzi wa Agosti Haki miliki ya picha AFP
Image caption Rais Ali Bongo akipiga kura katika uchaguzi wa Agosti

Uamuzi unatarajiwa Ijumaa au Jumamosi wa mahakama ya katiba Gabon kuhusu matokeo ya uchaguzi mkuu uliokumbwa na mzozo.

Mgombea aliyeshindwa Jean Ping amewasilisha kesi hiyo mahakamani akilalamikia udanganyifu.

Rais Ali Bongo alitangazwa mshindi wa uchaguzi huo wa Agoti 27 kwa tofuati ndogo ya chini ya kura 6000.

''Iwapo mahakama itageuza matokeo hayo, itakuwa mara ya kwanza mahakama inabatilisha matokeo ya uchaguzi wa urais baranai Afrika'', anasema Robert Gerenge, mkuu wa miradi maalum katika taasisi ya uchaguzi ya demokrasia endelevu Afrika.