'Utumwa wa watoto' Myanmar

San Kay Khine akionyesha alama na majeraha mikononi mwake Haki miliki ya picha AFP/Ye Aung Thuye Aung Thu
Image caption Mikono ya wasichana hao yana alama na majeraha

Rais wa Burma ameagiza uchunguzi ufanyike katika kesi ya wasichana wawili wanaosema waliwekwa kama wafungwa na kuteswa kwa miaka mitanoo katika duka la fundi cherehani.

Wasichana hao waliachiwa huru wiki iliopita baada ya muandishi habari kuwasaidia, lakini familia zao zinasema polisi ilikataa mara kadhaa kusikiza kilio chao.

Siku ya Jumatano na kesi hii ikigubika vyombo vya habari, Polisi hatimaye wamemkmata fundi huyo na jamaa zake wawili.

Wasichana hao wawili walikuwa na umri wa miaka 11 na 12 walipotumwa na wazazi wao katika mji mkuu kibiashara Yangon.

Kwa familia maskini Burma, nia uamuzi wenye uchungu na wa kawaida kwao. Umoja wa mataifa unkadiria kuwa watoto milioni moja wa Burma wanalazimishwa kuacha masomo na kufanya kazi.

Haki miliki ya picha AFP/Ye Aung Thuye Aung Thu
Image caption Wasichana hao sasa wanapokea matibabu nyumbani kwao, muelekeo wa maisha yao haujulikani

Wasichana hawa waligeuzwa wafanyakazi katika duka hilo la kushona. Lakini kilichoanza kama ajira ya malipo baadaye inatuhumiwa iligeuka kuwa utumwa. Wasichana hao wanasema hawakuruhusiwa kuwanona wazazi wao, hawakuruhusiwa kutoka na hatimaye hawakulipwa tena.

Alafu unyanyasaji ukaanza. Walipotembelewa na wanahabari wa shirika la AFP kijijiin mwao baada ya kuokolewa, walionekana na majeraha mikononi mwao ambayo wanasema yalitokana na mateso waliopata kutoka kwa waliowazuia.

"Nina jeraha nilipochomwa na pasi ya moto mguuni mwangu, na jeraha kichwani mwangu pia," moja ya wasichana hao mwenye umri wa miaka 16 sasa ameliambia AFP.

"Hapa nilichomwa kwa kisu, kwasababu sikupika chakula kizuri," alisema, akionyesha alama kwenye pua yake.

Msichana mwingine ambaye ana miaka 17 sasa alichomwa, alivunjwa vidole - adhabu anayosema aliyopewa na waliowafungia.

Haki miliki ya picha AFP/Ye Aung Thuye Aung Thu
Image caption Mama ya wasichana (katikati) anasema aliomba usaidizi kutoka kwa polisi mara kadhaa lakini hakusaidiwa

Tuhuma za kuteswa wasichana hao zinashutusha, lakini ni namna maafisa wa utawala walivyoshughulikia kesi hii ndio iliyowaghadhabisha wengi Burma.

Wengi wanaona kama ushahidi zaidi wa mfumo wa haki unaokandamiza maskini na wasiojiweza.

Maswali mengi sasa yanaulizwa kuhusu ni kwanini imechukua muda mrefu kwa maafisa kuhusika.

Rais Htin Kyaw ametoa taarifa rasmi akieleza kuwa ameagiza wizara husika kuwasaidia na kuwalinda wasichana, familia zao na muandishi Swe Win dhidi ya hatua zozote za kulipiza kisasi dhidi yao.

Muandishi Swe Win anatarajiwa kupewa tuzo ya rais kwa uchunguzi wake katika kesi hiyo.