Netanyahu amtaka rais wa Palestina kuhutubia bunge Israel

Netanyahu
Image caption Netanyahu

Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amemwalika kiongozi wa Palestina Mahmoud Abbas kulihutubia bunge la taiafa lake.

Bwana Netanyahu amesema kuwa pia yeye yuko tayari kulihutubia bunge la Palestina iwapo atapata mwaliko.

Alitoa matamshi hayo katika mkutano wa kila mwaka wa Umoja wa Mataifa,akimtaka Abbas kuzingatia amani badala ya ''kusababisha chuki''.

Bwana Abbas awali aliutaka Umoja wa Mataifa kutangaza mwaka 2017 kuwa kipindi ambacho Israel ilisitisha kukalia maeneo ya Palestina.

Ameutaka Umoja wa Mataifa kuidhinisha uhalali wa Palestina kisheria pamoja na kisiasa huku taifa hilo likipigania kuwa mwanachama kamili wa mashirika ya kimataifa.