Viongozi kujadili tatizo la maradhi sugu duniani
Huwezi kusikiliza tena

Viongozi wa dunia kukabiliana na changamoto za kiafya

Viongozi wa dunia wameahidi kuchukua hatua za pamoja kukabiliana na changamoto za kiafya, hasa usugu wa dawa unaotishia afya duniani. Wako katika mkutano mkuu wa Umoja wa Mataifa unaoendelea mjini New York. Ni mara ya tatu katika historia kwa mkutano huu kuzungumzia afya ya jamii, baada ya ugonjwa wa UKIMWI na Ebola. Usugu wa dawa hasa zinazotumika unazidi kuzua wasiwasi. Barani Afrika hali ni mbaya zaidi kwa nchi nyingi kwani utafiti wa kutosha haujafanyika kutathmini ukubwa wa janga hili. Mwandishi wa afya wa BBC Anne Soy ana taarifa hii kutoka Kilifi.