Wakristo na Waislamu waonyesha umoja Kibera Kenya
Huwezi kusikiliza tena

Wakristo na Waislamu waonyesha umoja Kibera Kenya

Makanisa na misikiti katika kitongoji duni cha kibera jijini Nairobi yanapata umbo jipya, baada ya kupakwa rangi ya manjano kama ishara ya umoja na uwiano baina ya waislamu na wakristo.

Mradi huo unaoendelezwa katika kitongoji duni cha kibera mjini Nairobi, ambacho ndiyo mojawapo ya mtaa mkubwa wa mabanda barani Africa, unalenga kuangamiza dhana ya ubabe wa kidini, unaosababisha mivutano na ugaidi miongoni mwa vijana kwa misingi ya dini.

Mradi huo, colour-in-faith unatumia sanaa kubadilisha jamii, na lengo la waasisi ni kuusambaza kote nchini Kenya

Anthony Irungu na taarifa zaidi.