Facebook 'imepitisha kima' cha waliotazama video zake

Facebook kwenye simu Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Facebook ilipuuza video fupi zilizotazamwa

Facebook imepitisha idadi ya watu waliotazama video katika mtandao huo katika miaka miwili iliyopita kampuni hiyo imekiri.

Mteja mmoja anayetangaza biashara katika mtandao huo amesema kwa wakatimwingine, takwimu hizo zilipitishwa kwa hadi 80%.

Facebook's analytics ni kigezo wanachotumia wafanyabiashara wanaotangaza biashara zao kubaini ni kiasi gani video zao zinatizamwa kwenye Facebook.

Mtandao huo wa kijamii unasema makosa hayo yamerekebishwa na hayajabadili kiwango wanacholipa wafanyabiashara kutangaziwa biashara zao.

'Mwenendo usiokubalika'

Katika taarifa yake, Facebook imesema: "Tumegundua hivi karibuni makosa katika namna tunavyohesabu idadi ya watu wanaoangalia video.

"makosa haya yamerekebishwa, haikuathiri malipo na tumewaarifu washirika wetu," imeongeza.

Kifaa hicho cha kuhesabu kimebadilishwa jina kwa sasa na kimepewa jina "average watch time" na Facebook imeanza kukitumia kukusanya takwimu za watu wanaotizama video mwishoni mwa mwezi agosti.

Jarida la Wall Street limeinukuu kampuni ya Publicis iliosema kuwa Facebook kutoa takwimu za makosa "haikubaliki".

Publicis imesema inaonyesha haja ya kuwa na kampuni ya tatu kuangalia upya takwimu zinazokusanywa na Facebook.

Mtandao huo wa kijamii umewahi kushutumiwa tena katika siku za nyuma kwa kuhesabu video inatazamwa baada ya sekundi tatu tu .

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii