Msichana mdogo atangazwa chifu Nigeria

Msichana Hindatu Umar
Image caption Chifu wa mji wa Argungu ulioko kazkazini magharibi mwa Nigeria, Hindatu Umar aliye na umri wa miaka 25

Msichana mmoja mwenye umri wa miaka 25 ametangazwa kuwa chifu wa mji Argungu wa kazkazini magharibi mwa Nigeria, ikiwa ni mara ya kwanza wanamke kushika wadha huo.

Hindatu Umar pia anakuwa chifu mwenye umri mdogo zaidi kuwahi kuwa chifu wa mji huo katika jimbo la Kebbi lenye wakaazi wengi waislamu.

Baadhi ya wakaazi wa eneo hilo wamelalamika wakidai hana ujuzi wa kutosha na si mkakamavu.

Lakini ukweli ni kwamba amekuwa akihudumu kama naibu wa chifu kwa mda sasa ndiposa akapandishwa cheo baada ya mda wa aliyekuwa chifu kumalizika.

Mwandishi wa BBC katika eneo hilo anasema wengi wameshangazwa na hatua hiyo kwa sababu ni nadra kwa wanawake kushika nyadhfa za kiutawala na kisiasa katika maeneo yaliyo na waakaazi wengi waislamu huko kazkazini mwa Nigeria.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii