3 wapigwa risasi na kuuawa Burlington Marekani

Maduka ya Cascade Mall Burlington Marekani Haki miliki ya picha AP

Polisi katika jimbo la Washington nchini Marekani wanasema kuwa watu watatu wamepigwa risasi na kufariki na wengine wawili kujeruhiwa vibaya.

Wanasema shambulio hilo lilitokea katika eneo la Burlington, mwendo wa saa moja hivi kutoka mji wa Seattle.

Shambulio hilo lilitekelezwa Ijumaa alasiri katika maduka ya Cascade Mall.

Awali polisi walisema kuwa ni watu wanne waliokuwa wameuawa kwa kupigwa risasi lakini kwa sasa wameeleza kuwa wanawake watatu walipatikana wameuawa katika maduka ya Macy na mwanamume mmoja amepelekwa hospitalini akiwa na majeraha mabaya.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Polisi wamechapisha picha hii ya mshukiwa

Ilichukua muda wa saa kadhaa kabla ya eneo hilo kutangazwa kuwa salama tena kabla ya wauguzi kuruhusiwa kuingia ndani kuwahudumia watu waliokuwa wamejeruhiwa.

Polisi wamechapisha picha ya mshukiwa huyo wa kipekee ambaye wamemtaja kuwa mwenye asili ya Uhispania, aliyeonekana akibeba bunduki.

Kulingana na polisi alionekana mara ya mwisho akitembelea kuelekea kwenye barabara kuu.

Watu katika eneo hilo wameshauriwa wasalie ndani ya nyumba zao na wafunge milango.