Mashambulizi yasababisha ukosefu wa maji Aleppo

Raia watalazimika kutumia maji machafu UNICEF linasema Haki miliki ya picha Reuters

Waokoaji wanaofanya kazi katika eneo linalothibitiwa na waasi la Aleppo wanasema kuwa mashambulizi ya ndege katika eneo hilo yamepamba moto.

Wafanyakazi watano wa kutoa misaada wamejeruhiwa huku ndege za jeshi za Serikali zikiendelea kushambulia mji wa Aleppo.

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuwashughulikia watoto, UNICEF, limesema kuwa pampu ya kutoa maji ya Aleppo imeharibiwa.

Pampu hiyo huwashughulikia zaidi ya watu milioni moja wa Aleppo.

Shirika hilo linasema mapigano hayo yamezuia juhudi zozote za kufanyia marekebisho pampu hiyo.

Haki miliki ya picha Reuters

Hakuna mapumziko yoyote kwa watu wa Aleppo.

Watu wa kujitolea wanasema kuwa mashambulizi ya ndege yalianza mapema Jumamosi asubuhi na mamia ya watu wamekwama katika vifusi, huku hospitali zikishindwa kuwatosheleza wote waliojeruhiwa.

Mashambulizi hayo si ya kubahatisha kwa sababu yameonekana kulenga mijengo, hatua ambayo imevuruga maisha ya kawaida katika eneo hilo.

Mashambulizi hayo ya Serikali ya Libya na Urusi yaliharibu kabisa pampu ya maji katika eneo hilo la Aleppo.

Watu 250,000 wanategemea maji hayo.

UNICEF limesema kuwa wakaazi wa eneo hilo watalazimika kutumia maji machafu ya chumvi na kuta kuwa na hatari ya kupata maradhi yanayosambazwa na maji.

Katika kulipiza kisasi, kituo kinachosambazia maji watu milioni 1.5 magharibi mwa mji huo yalikatwa.

Image caption Wengi wanaendelea kuathirika na mapigano Syria

Hata hivyo UNICEF wamesema kuwa watajaribu kupata maji safi katika visima vya chini kabisa.

Inasemekana kuwa watu 91 waliuawa katika mashambulizi ya Ijumaa na mijengo 41 iliharibiwa.

Jeshi la Syria linasema kuwa linajiandaa kuanzisha mashambulizi ya chini kwa chini na limeshauri wananchi kujiondoa katika maeneo yanayosema ni ya kigaidi.