Simu ya Samsung yafuka moshi ndani ya ndege

Simu ya Samsung iliokuwa ikifuka moshi ndani ya ndege
Image caption Simu ya Samsung iliokuwa ikifuka moshi ndani ya ndege

Wafanyikazi wa kampuni moja ya ndege nchini India walilazimika kutumia kifaa cha kuzima moto ili kuizima simu aina ya Samsung iliokuwa ikifuka moshi.

Simu hiyo ya Note 2 ilikuwa ikitoka miale ya moto kulingana na taarifa kutoka kwa kampuni ya ndege ya Airline Indigo.

Hatua hiyo ya haraka iliochukuliwa na wafanyikazi hao ilisaidia ndege hiyo kutua salama katika uwanja wa ndege wa Chennai,ikiwa ndio lengo la safari hiyo.

Kisa hicho kimetokea wakati ambapo Samsung inazirudisha simu aina ya Note 7 kutokana na matatizo ya betri.

IndiGo imesema kuwa hakuna mtu aliyejeruhiwa wakati wa kisa hicho katika ndege ya 6E-054 iliokuwa ikitoka Singapore kuelekea Chennai.