Polisi watoa video ya kuuawa kwa Scott

Huwezi kusikiliza tena
Video iliyotolewa na polisi

Familia ya mwanamme mweusi Keith Lamont Scott aliyeuawa wanasema ushahidi wa video uliotolewa na polisi imewaacha na maswali mengi zaidi ambayo polisi wameshindwa kujibu.

Video hiyo imetolewa Baada ya siku kadhaa za maandamano makali ya raia weusi wa Marekani ya kupinga mauaji ya dhuluma katika tukio jingine la polisi kumfyatulia risasi na kumuua mwenzao huko Charlotte Jumanne iliyopita.

Katika video hiyo inawaonyesha polisi wakilenga gari la mwanamme huyo Keith Scott, ambae kisha wanafyatulia risasi mara nne baada ya kutoka nje ya gari na kurudi nyuma.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Polisi walitoa picha ya bastola ambayo wanadai bwana Scott alikuwa nayo

Haibainiki vyema kama marehemu Scott alikuwa na bunduki kama polisi wanavyodai lakini wanasema bado wanaendelea na uchunguzi wao.

Familia ya Scott imekuwa ikisisitiza kwamba Scott hakuwa na silaha yoyote.

Huwezi kusikiliza tena
Video iliyonaswa na mkewe Scott

Mkewe Scott alikuwa wa kwanza kutoa video ya tukio hilo, kuonyesha kuwa mumewe aliuawa na polisi bila kuwa na hatia yoyote. Maanaharakati wa haki za kibinadamu Jesse Jackson, amesema kuna kila ishara kwamba polisi wanalengo la kuficha ukweli wa dhuluma hiyo

Image caption Keith Lamont Scott (kulia) na Polisi aliyemuua Brently Vinson (kulia)