Mashambulizi ya Aleppo kuzungumziwa UN

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Ndege za serikali zimekuwa zikishambulia maeneo ya mji wa Aleppo

Baraza la usalama la umoja wa mataifa linatarajiwa kufanya mkutano wa dharura kwenye mda wa saa chache zijazo kuzungumzia hali ya vita vinavyozidi kurindima huko mjini Aleppo nchini Syria.

Uingereza, Ufaransa na Marekani wameitisha kikao hicho baada ya Vikosi vya majeshi ya serikali ya rasi Bashar Al Asaad kuziidisha mashambulio dhidi ya washindani wao tangu kuvunjika kwa mkataba wa kusitisha mapigano wa hivi majuzi.

Wanaitaka Urusi kuishawishi serikali ya Syria kutofanya mashambulio ya angani kiholela.

Huwezi kusikiliza tena
Mtoto akiokolewa wakati wa siku ya pili ya mashambulizi

Zaidi ya watu 40 wameripotiwa kufariki hapo jana pekee.

Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza , Boris Johnson, amenukuliwa kusema huenda urusi ilihusika kimaksudi na shambulio la msafara wa watoa huduma za kibinadamu hapo juzi, na kwamba lichukuliwe kuwa uhalifu wa kivita . Urussi wamekana kuhusika na shambulio hilo.