Bongo kujumuisha upinzani ndani ya serikali

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Bongo amesema atajumuisha upinzani bungeni

Katika hatua inayoonekana kujaribu kupunguza utesi na hisia kali zilizotokana na uchaguzi tata nchini Gabon,Rais Ali Bongo ,amesema uteuzi wa baraza lake la mawaziri litajumuisha wanasiasa wa vyama vingine.

Bwana Bongo amefafanua kuwa japo ana mipango hiyo ya kuwajumuisha wanachama wa upinzani katika serikali yake kiongozi wao ,Jean Ping, amekataa mazungumzo naye.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Jean Ping(katikati)

Bwana Ping amepinga matokeo ya uchaguzi yaliyomtangaza Ali Bongo kama mshindi na kushutumu uamuzi wa mahakama ya kikatiba nchini humo iliyoidhinisha matokeo hayo.

Watu kadhaa walifariki mwezi uliopita kutokana na vurugu za baada ya uchaguzi wa Gabon.