Shekau: Niko hai na salama

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Shekau anasema kuwa yuko salama

Kiongozi anayekabiliwa na upinzani wa kundi la Nigeria Boko Haram Abubakar Shekau, ametoa kanda ya video akikana madai ya jeshi kuwa aliuawa au amepata majeraha mabaya wakati wa mashambulizi ya angania mwezi uliopita.

Shekau alionekana mwenye afya kwenye kanda hiyo ambayo alizungumza kwa lugha za kiarabu,Hausa na Kanuri.

Haijabainika video hiyo ilirekodiwa lini. Bado jeshi la Nigeria halijazungumza chochote.

Mapema mwezi huu kundi la Islamic State ambalo Boko Haram limetangza kulitii, lilitangaza kuwa wadhifa wa Shekau ulikuwa umechukuliwa na kiongozi asiye maarufu Abu Mus'ab Albarnawi. Bado Shekau anasema kuwa ndiye kiongozi.