Trump atishia kumualika mpenzi wa zamani wa Clinton

Image caption Trump atishia kumualika aliyekuwa mpenzi wa Clinton

Donald Trump ametishia kumualika mwanamke ambaye alikuwa mpenzi wa Bill Clinton akiwa kwenye ndoa na Hillary Clinton.

Trump amesema atamualika Gennifer Flowers akae mbele kabisa, kwenye mjadala baina yake Trump na mpinzani wake wa kugombea urais, Hillary Clinton, hapo kesho.

Bwana Trump alisema hayo, kujibu matamshi ya bilioneya anayeshindana naye, Mark Cuban ambaye alisema, kampeni ya Clinton imempa kiti cha mbele katika mjadala huo.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Gennifer Flowers anadai alikuwa mpenzi wa Bill Clinton akiwa kwenye ndoa na Hillary

Gennifer Flowers, mrembo wa zamani, amejibu kwenye Twitter, kwamba amepokea mualiko wa Bwana Trump.

Haijulikani kama Trump atafuata tishio lake hilo au la.