Watu 17 wafa wakihofia kuvamiwa na waasi DRC

Image caption Wengi walizama maji huku wengi wakipatwa na mshtuko wa moyo.

Takriban watu 17 wameaga dunia katika mji wa Beni ulio nchini Jamhuri ya Demokrasi ya Congo, waliposhikwa na uoga na wakaanza kukimbia wakifikiri kuwa walikuwa wakishambuliwa na kundi la waasi.

Wenyeji walidhani kuwa walikuwa wamevamiwa na kundi la waasi ambalo huwaua raia eneo hilo

Wengi walizama maji huku wengine wakipatwa na mshtuko wa moyo.

Ripoti zinasema kuwa hali ilibadilika na kuwa mbaya zaidi wakati mwanajeshi aliyekuwa amevaa kama raia alianza kurusha risasi hewani

Wakaazi wa mji wa Beni wanadaiwa kufikia kuwa kundi la waasi ambalo mara kawa mara huwaua watu mjini humo lilikuwa limewasili.

Wanaharakati wanasema kuwa zaidi ya watu 1000 wameuawa katika kipindi cha miaka miwili iliyopita na kundi la Allied Democtartic Forces kutoka nchini Uganda.