Polisi wamethibitisha bomu la kienyeji lilisababisha mauaji ya wenzao nchini Hungary

Ofisa wa polisi aliyekuwa kwenye doria akitembea kwa miguu alilengwa na shambulio hilo
Image caption Ofisa wa polisi aliyekuwa kwenye doria akitembea kwa miguu alilengwa na shambulio hilo

Polisi nchini Hungary wanasema mlipuko wa Budapest usiku wa Jumamosi uliowajeruhi maafisa wawili wa polisi ulisababishwa na bomu la kienyeji.

Mkuu wa jeshi la polisi wa Hungary Karoly Papp amesema ofisa wa polisi aliyekuwa kwenye doria akitembea kwa miguu alilengwa na shambulio hilo.

Kwa sasa wapo katika hali nzuri wakiwa hospitalini.

Image caption Mshukiwa wa shambulizi hilo bado anatafutwa

Mtu anayeshutumiwa kutekeleza shambulizi hilo, anaelezewa kuwa ni kijana wa miaka ishirini, bado hajapatikana.