Tamasha la kutatanisha lafungiwa nchini Urusi

Mashuhuda wanasema takriban wanaharakati ishirini waliojiita kuwa ni maafsa wa Urusi, walilifunga tamasha hilo mjini Moscow
Image caption Mashuhuda wanasema takriban wanaharakati ishirini waliojiita kuwa ni maafsa wa Urusi, walilifunga tamasha hilo mjini Moscow

Tamasha nchini Urusi la mpiga picha anyetatanisha wa marekani limefungwa baada kupingwa na wanaharakati.

Picha ziliyopigwa na Jock Sturges inajumuisha picha zinazomwonyesha mtoto akiwa mtupu.

Seneta wa kihafidhina mwenye ushawishi mkubwa na mshauri wa serikali kwa masuala ya watoto wote wamelielezea tamasha hilo kuwa ni tamsha la ngono ya watoto na wametaka kufungwa kwake.

Mashuhuda wanasema takriban wanaharakati ishirini waliojiita kuwa ni maafsa wa Urusi, walilifunga tamasha hilo mjini Moscow na mmoja kati yao alirembea chupa ya mkojo juu ya baadhi ya picha hizo.

Msimamizi wa tamasha hilo alisema alikuwa analifunga tamasha hilo baada ya kupata vitisho kwa watu wenye nia mbaya.