Somalia: Wapiganaji wa al-shabab washindwa kijeshi

Miundombinu na majengo vimeharibiwa vibaya na vita
Image caption Miundombinu na majengo vimeharibiwa vibaya na vita

Waziri wa mambo ya nje wa Somalia, Abdisalam Hadliyeh anasema kundi la wapiganaji wa kiislamu la Al Shabaab limeshindwa kijeshi, kwa ushirikiano wa jeshi la Somalia na vikosi vya kulinda amani vya umoja wa Afrika.

Waziri huyo amesema Al Shabaab kwa sasa wanamiliki chini ya asilimia kumi ya nchi nzima , na viongozi wake wengi wameuwawa au kukimbia katika miezi ya hivi karibuni.

Hadliyeh amesema kuwa jambo lililopelekea utulivu wa muda mrefu ni kuwa na vifaa vizuri, mafunzo ya kijeshi na kufadhiliwa vikosi vya usalama vya taifa.

Mchambuzi wa BBC wa masuala ya Afrika anasema kwamba licha ya kuwa kundi hilo limetokomezwa kwenye mji mkuu wa Mogadishu, lakini bado linaendesha mashambulizi ya mara kwa mara mjini hapa na kwengineko.