Msanii kutoka Ethiopia akimbia na kuomba hifadhi Marekani

Image caption Vikosi vya Ethiopia vinalaumiwa kwa kuendesha dhuluma dhidi ya raia

Msanii maarufu nchini Ethiopia ameomba hifadhi nchini Marekani kutokana na kile alichokitaja kuwa dhuluma zinazoendeshwa na vikosi vya usalama.

Znah-Bzu Tsegaye, ambaye ameshiri katika filamu kadha nchini Ethiopia anatoka kabila la Amhara. Makabila ya Amhara na Oromo ambayo ndiyo makubwa zaidi nchini Ethiopia yamekuwa yakifanya maandamano ya kuipinga serikali kwa miezi kadha.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Feyisa Lilesa alifanya ishara ya kuipinga serikali wakati mashindanoo ya Olimpiki

Bwana Znah-Bzu ndiye mtu maarufu kuikimbia nchi siku za hivi majuzi. Wakati wa mashindano ya Olimpiki mwanariadha kutoka jamii ya Oromo aliamua kutorudi nyumbani nyumbani baada ya kufanya ishara ya kuipinga serikali.