Mchezaji wa Ivory Coast afungwa miezi 2 jela Ufaransa

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Serge Aurier alifungwa miezi miwili na faini ya dola 674

Mcheza kandanda raia wa Ivory Coast Serge Aurier, ambaye anaichezea klabu ya Paris St-Germain (PSG), amehukumiwa kifungo cha miezi miwili jela kwa kumgonga afisa wa polisi.

Aurier pia alipigwa faini ya dola 674 kutokana na kisa hicho kilichotokea kwenye klabu ya burudani mwezi Mei mjini Paris.

Hata hivyo atabaki kuwa huru akisubiri rufaa, ikiaamsiha kuwa nawza kuichezea PSG katika ligi ya mabingwa siku ya Jumatano.