Wanawake wapinga kusindikizwa na wanaume nchini Saudi Arabia

Haki miliki ya picha AZIZA AL-YOUSEF
Image caption Mwanamke ni lazima apate ruhusa ya kusindikizwa na mwanamme ili aweze kusafiri nchi za nje

Azimio lililotiwa sahihi na zaidi ya wanawake 14,000 nchini Saudi Arabia la kumaliza mfumo wa wanawake kusindikizwa na wanaume limewasilishwa kwa serikali.

Mwanamke ni lazima apate ruhusa ya kusindikizwa na mwanamme ili aweze kusafiri nchi za nje na mara nyingi uhitaji idhini kuweza kufanya kazi au kusoma.

Mwanaharakati Aziza Al-Yousef ambaye aliwasilisha azimio hilo aliiambia BBC kuwa anajivunia kuchukua hatua hiyo lakini sasa anasubiri majibu.

Haki miliki ya picha AZIZA AL-YOUSEF
Image caption Aziza Al-Yousef anasema anajivunia kuwasilsisha azimio hilo

Katika taifa hilo la kiislamu, mwanamke anastahili kupata ruhusa kutoka kwa babake, nduguye au mtu mwingine mwanamme kutoka familia, kama yeye ni mjane kwa mafano mtoto wake wa kiume, kuweza kupata cheti cha kusafiri, kuolewa au kuondoka nchi hiyo.

Kukodisha nyumba, kupata matibabu hospitalini na kupeleka kesi mahakamani mara nyingi uhitaji ruhusa ya mwanamme.