Uyoga watunza msitu wa Nou
Huwezi kusikiliza tena

Uyoga watunza msitu wa Nou

Tanzania ni miongoni mwa nchi kumi zinazopoteza misitu kwa kasi duniani kulingana na takwimu za benki ya dunia (world bank) na wanasema ikiendelea kwa kasi hiyo kwa miaka hamsini ijayo, Tanzania itakuwa haina misitu tena.

Lakini katika msitu wa Nou uliopo Manyara,kaskazini mwa Tanzania,baadhi ya wanakijiji wanaouzunguka msitu huo wameanzisha mbinu ya kutumia uyoga kama njia mbadala ya kujipatia kipato na kuokoa msitu huo.