Italia kupiga kura ya mabadiliko ya katiba mwezi Desemba

Renzi anasema lengo la mabadiliko hayo ni kusaidia kuepuka msuguano wa kisiasa
Image caption Renzi anasema lengo la mabadiliko hayo ni kusaidia kuepuka msuguano wa kisiasa

Raia wa Italia watapiga kura ya mabadiliko ya katiba mnamo tarehe nne Desemba. Kama watakataa, basi waziri mkuu Matteo Renzi, amesema atajiuzulu.

Anasema mabadiliko hayo ya katiba yataboresha mfumo wa kisiasa wa Italia kwa kupunguza nguvu ya seneti na kuondoa ushawishi wa kikanda.

Bwana Renzi anasema lengo la mabadiliko hayo ni kusaidia kuepuka msuguano wa kisiasa lakini upinzani unahofu kuwa mabadiliko hayo yataipa serikali mamlaka makubwa.

Mwandishi wa BBC anasema kuwa kura hiyo ya mabadiliko ya katiba inatengeneza hatari zaidi ya kutokea mtafaruku wa kisiasa barani Ulaya.