Mwanazuoni wa Iran aachiliwa gerezani

Ameachiliwa huru kutokana na sababu za maradhi
Image caption Ameachiliwa huru kutokana na sababu za maradhi

Shirika la habari la Iran linasema kuwa mwanamke mmoja mwanazouni mzaliwa wa Iran mwenye asili ya Canada ameachiliwa huru kutoka gerezani kwa misingi ya kibinaadam.

Homa Hoodfar, Profesa mstaafu alikamatwa mjini Tehran mwezi Juni.

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ameliambia shirika hilo la habari kwamba mwanamama huyo ameachiliwa huru kutokana na sababu za maradhi, na kwamba alikuwa njiani kurudi Canada akipitia oman.

Familia ya Bi Hoodfar inasema kuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa mishipa ya fahamu.

Mwanazuoni huyo mstaafu alikuwa ni mmoja ya watu wengi wenye uraia pacha amabo wanashikiliwa nchini iran kwa tuhuma za vitendo vya kuhatarisha usalama wa taifa.