Al Mahdi kuhukumiwa mahakama ya ICC

Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita (ICC) inatarajiwa kutoa hukumu dhidi ya mwanamgambo wa Kiislamu raia wa Mali Ahmad Al Faqi Al Mahdi.

Al-Mahdi ameshtakiwa makosa ya uhalifu wa kivita kuhusiana na kuharibiwa kwa makaburi tisa na msikiti mashuhuri katika mji wa kale wa Timbuktu, 2012.