Ramani inayowezesha gari kupata sehemu ya kuegesha

Magari yenye ramani ya kidijitali
Image caption Magari yenye ramani ya kidijitali

Magari aina ya Audi,BMW na Mercedes Benz yalio na sensa yatakuwa yakigawana habari kuhusu maeneo ya kuegesha magari na marekebisho ya barabara kupitia huduma ya ramani ya kidijitali.

Pia magari hayo yatakusanya data kuhusu mazingira ya msongamano wa magari ,hatari na ishara za barabarani.

Huduma hiyo inayotolewa na kampuni ya Mapping inayomilikiwa na kundi moja la watengezaji magari itaanza mwaka ujao.

Huduma hiyo itarekodi kasi ya magari,eneo la gari,mwelekeo, breki za ghafla na taa za ukungu.

Image caption Magari ya kidijitali

Picha za video za hatari iliopo barabarani pia zitaonekana na kamera inayoangalia mbele.

Wamiliki wa magari hayo hawatafanya lolote kupokea ama kusambaza data, lakini watalazimika kuingia katika programu hiyo kwa kutumia simu aina smartphone .