Asali ''inaweza kukabili maambukizi ya mkojo''

Asali hukabiliana na maambukizi ya mkojo
Image caption Asali hukabiliana na maambukizi ya mkojo

Asali na maji inaweza kutumika dhidi ya maambukizi ya mikojo katika wagonjwa waliolazwa hospitalini,watafiti wa Uingereza wamesema.

Wagonjwa huwekewa bomba linalotumika kutoa mikojo iliokwama katika kibofu cha mkojo ama hata kuchunguza kiwango cha mikojo kinachotoka katika mwili wa mwanadamu.

Lakini mabomba hayo mara nyengine yanaweza kusababisha maambukizi.

Wanasayansi katika chuo kikuu cha Southampton wameonyesha katika maabara kwamba asali ilio majimaji huzuia baadhi ya bekteria kutotengeza mapande yalio magumu kuondoa ndani ya plastiki.

Image caption Mfuko wa mkojo unaowekewa mgonjwa aliyelazwa hospitalini

Asali husaidia katika kusafisha mabomba hayo na kuyaweka safi wakati ambapo yameshikana na vibofu vya mkojo.

Hatahivyo majaribio mengi yatahitajika ili kubaini iwapo ni salama kutumia kwa binaadamu.