Boko Haram wateka vijiji na kupandisha bendera Nigeria

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Boko Haram wametangaza kulitii kundi la Islamic State

Wanamgambo wa kiislamu nchini Nigeria Boko Haram wametundika bendera kwenye vijiji vitatu vilivyo Kaskazini mashariki mwa nchi baada ya kuchukua udhibiti wa vijiji hivyo jana jumatatu.

Wanamgambo hao waliwaua kwa kuwachinja watu wanane akiwemo kiongozi wa kijiji wakati wa shambulizi hilo.

Vijiji vya Kubirivour, Boftari na Kuburmbalah viko karibu na mji wa Chikok ambapo wanamgambo hao walewateka zaidi ya wasichana 200 wa shule mwaka 2014.

Wengine wanasema kuwa wanamgambo hao bado wanadhibiti mji wa Malan Fatyori ulio kwenye mpaka kati ya Nigeria na Niger.

Jumapili iliyopita wanajeshi wa Nigeria waliutwaa mji huo kutoka kwa wanamgambo. Hata hivyo wanamgambo hao walijiandaa na kuudhibiti tena mji huo.