Senegal yazuiwa kutwaa mali ya mtoto wa Wade

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Karim alikuwa mshauri mwenye ushawishi na waziri wakati wa utawala wa babake kati ya mwaka 2000 na 2012.

Mahakama nchini Ufaransa imekataa ombi la serikali ya Senegal la kutaka kutwaa mali ya waziri wa zamani Karim Wade ikiwemo nyumba ya kifahari iliyo mjini Paris na akaunti yake ya benki na kusema kuwa haikutapa ushahidi wa kutosha kuhusu ufisadi.

Jean-Marc Fediba, mmoja wa mawakili wanaomuakilisha mtoto wa rais wa zamani Abdoulaye Wade alivyambia vyombo vya habari kuwa huo ni ushahidi kuwa alihukumia kimakosa kifungo cha miaka sita jela nchini Senagal.

Karim Wade aliachiliwa mapema mwaka huu baada ya kutumikia kifungo cha miaka 2 jela. Hata hivyo serikali inasema kuwa anahitaji kulipa dola milioni 225.

Karim alikuwa mshauri mwenye ushawishi na waziri wakati wa utawala wa babake kati ya mwaka 2000 na 2012.