Matokeo ya mechi za ligi ya mabingwa Ulaya

Leicester city Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mshambuliaji wa timu ya Fc Porto Adrian Lopez, akiwa katikati ya msitu wa walinzi wa timu ya Leicester city

Leicester city wakicheza katika dimba lao la king power wameibuka na ushindi wa pili katika michuano ya ulaya kwa kuichapa FC Porto kwa bao 1-0.

Real madrid wakicheza ugenini katika dimba la Signal iduna Park wametosha nguvu na wenyeji Borrusia Dortmund kwa kufunga mabao 2-2. Nao Monaco wakavutwa shati nyumbani kwa sare ya bao 1-1 na Bayer Leverkusen.

Wareno wa Sporting Lisbon wamewalaza Legia Warszawa toka Poland kwa mabao 2-0 FC Copenhagen wameibuka na ushindi wa kishindo wa mabao 4-0 dhidi ya Club Brugge

Vibibi vizee wa Turin Juventus wameibuka na ushindi ugenini kwa kuichapa Dinamo Zagreb mabao 4-0,Sevilla wameshinda 1-0 dhidi ya Lyon huku Tottenham ikichomoza na ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji CSKA Moscow.