Dawa ya watoto ya kutibu kifua kikuu yazinduliwa Kenya

Dawa ya watoto ya kutibu kifua kikuu yazinduliwa Kenya

Dawa ya kwanza duniani kuwahi kutengenezwa ili kutibu watoto wanaougua maradhi ya kifua kikuu imezinduliwa leo mjini Nairobi.

Ni tembe yenye ladha tamu inayotarajiwa kuimarisha matibabu ya kifua kikuu na kuokoa maisha ya watoto wengi wanaoambukizwa.

Kenya ni nchi ya kwanza duniani kununua dawa hizo na kuzisambaza kote nchini. Takriban nchi 20 tayari zimeanza kuunda sera zitakazowawezesha kununua dawa hizo mpya.

Mwandishi wa BBC wa masuala ya afya Anne Soy ana taarifa hiyo kutoka Nairobi